Quantcast
Channel: Mbeya Yetu
Viewing all 1224 articles
Browse latest View live

MUHIMU SANA: USAILI WA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA WAKAZI WA MBEYA

$
0
0


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.

Muhimu:

Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.

• Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s) ], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

• Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..

• Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI
01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.



TANGAZO! TANGAZO : JE UNATAFUTA NYUMBA YA KUPANGA, CHUMBA CHA BIASHARA, KUNUNUA, GARI YA KUNUNUA AU KUKODI, MSICHANA WA KAZI, MASHAMBA NA MENGINEYO ? JIBU HILI HAPA.

$
0
0
ZAMA REAL ESTATES, JOBS, & ADVERTISEMENTS AGENCY

Tupigie kupitia simu namba +255754060350, +255686957255.

BlogSpot:matangazombeya.blogspot.com,Email:matangazombeya@yahoo.com/Face:Book:matangazombeya@facebook.com. Ofisi zetu zipo Mama John,Mbeya.

JE UNATAFUTA NYUMBA YA KUPANGA, CHUMBA CHA BIASHARA, KUNUNUA, GARI YA KUNUNUA AU KUKODI, MSICHANA WA KAZI? KAMA NDIO WASILIANA NA ZAMA REAL ESTATES, JOBS & ADVERTISEMENTS AGENCY. WATAKUPA MSAADA WA HARAKA ZAIDI!!!!!!! 

 Magari:-Sale & Rent Cars
Magari yaliyotumika yanauzwa na kukodishwa. Bei zake ni maelewano na wahusika wenyewe.

Magari yaliyopo mikononi: Harrier, Prado, Hiace, Land crusa, Costa, Corola, Mark 11, Canter, pikipiki, Bajaji nk. Pia tuna magari yanakodishwa kwa ajili ya safari za kikazi na kifamilia kwa bei nafuu kabisa!!

 Nyumba za Kupanga:- House Rent
Nyumba hizi zipo maeneo mbalimbali kama vile Sai, Ilomba, VETA, Forest Mpya, Soweto, Block T, Jakaranda, Uhindini, Uzunguni nk.

Gharama za nyumba zinatofautiana kutokana na mahali zilipo na ukubwa wa nyumba  hizo. kuna baadhi ya nyumba zina kila kitu ndani (full furnished) . Endapo una nyumba ya kupangisha , tafadhali usisite kuwasiliana nasi ili tukusaidie kukutafutia wapangaji.


Nyumba za kuuzwa:- House for Sale

Tuna nyumba zinauzwa maeneo mbalimbali kama vile Sai, Ilomba,  Forest  New and Old, VETA, Soweto, Block T, Jakaranda, Uhindini, Uzunguni , Mama John , nyumba za barabarani maalum kwa ajili ya biashara, kama vile hotel, maduka, Bank, Guest House,  sheli, nk. Bei hizi zinatofautiana kulingana na ubora wa nyumba, Ukubwa, Thamani, Eneo nk. Pia kuna nyumba zilizopo kwenye kona. (Nyumba zilizojengwa kwenye kona zina matumizi mengi mazuri kibiashara). Endapo una nyumba ya kuuza, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.


DO YOU NEED TO BUY OR RENT A HOUSE, SHOP, OFFICE, BUY & RENT A CAR, PLEASE DO NOT HESTATE TO CONTACT ZAMA REAL ESTATES, JOBS & ADVERTISEMENTS AGENCY


Ni mawakala/Madalali wenye uwezo wa kukutafutia nyumba za kupanga, nyumba za kununua, Mashamba, Viwanja, Yadi, Ofisi, Magari nk, Hotel na Guest houses. kwa bei poa kabisa.



Viwanja/Plots

Vinanja vinauzwa maeneo mbalimbali kama vile VETA, Ilomba, Pipeline, Forest Mpya, Iwambi, Ituha , Block T, Mkuranga,  nk. Kuna baadhi ya viwanja vimepimwa na vingine havijapimwa. Bei zake zinategemeana na eneo kilipo na ukubwa wa kiwanja. Bei zake zinaanzia Tshs. 4M  na kuendela. Viwanja hivi baadhi vipo barabara kuu ya TANZAM. Endapo una kiwanja unauza tafadhali usisite kuwasiliana nasi.


Mashamba/Land

Mashamba yapo maeneo ya Mbozi, Tunduma, Tukuyu, Mpemba, Mkuranga, nk. Endapo una shamba usisite kuwasiliana nasi ili tukuuzie.


Ofisi:-Offices

Majengo   yanayofaa kwa  ajili ya  matumizi ya Ofisi yanapangishwa maeneo mbalimbali jijini Mbeya. Gharama zinatofautiana kutokana na eneo  na ukubwa wa ofisi .


Yadi/Viwanda, Ghala kubwa

Kuna majengo  na viwanja vikubwa vinayyofaa kwa ujenzi wa Yadi au viwanda vyenye squre meter zaidi ya 3,000.



Guest houses na Hotels

Guest houses na Hotel zinauzwa maeneo mbalimbali jijini Mbeya. Endapo unahitaji usisite kuwasiliana nasi.


Sheli:-

Vituo vya mafuta vinauzwa maeneo mbalimbali jijini Mbeya


Matangazo ya Biashara

Tunajishughulisha  na matangazo ya Biashara kupitia kwenye Blog yetu. Matangazo ya aina yoyote kwa kutuma kwenye email address yetu, au anuani.


Ajira

Tuna warembo na vijana wenye umri chini ya miaka 25 wenye uwezo wa kutangaza biashara yako. Au kwa kuajiriwa kwenye mahotel, clubs, Pub, Bar , watumishi wa nyumbani nk. Wengi wa vijana hawa wamesoma hadi kidato cha nne, wanazungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha! Hadi sasa tumefanikiwa kuwatafutia wasichana na wavulana kazi mbalimbali.


Ushauri 

Tunatoa ushauri kwa waliotingwa na msongo wa mawazo(hii ni siri),


Tiba Asili.

Tunatibu kupitia Tiba Asilia zinazotumia vyakula na Mimea, magonjwa ya Tumbo, Pressure, Kisukari, Malaria sugu, Typhoid, magonjwa ya ngozi, Fangasi, pia tuna hair products zenye uwezo wa kurefusha na kuboresha nywele zako kwa muda mfupi sana, kuondoa mba nk.


Marafiki /Wachumba club

Tunawaunganisha wasichana na wavulana wanaotafuta wachumba au marafiki kupitia kwenye blogspot yetu

Kwa bei nafuu sana

Unaweza pia kututembelee kwenye blogspot yetu ya matangazombeya.blogspot.com

Wote mnakaribishwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Tupigie kupitia simu namba +255754060350, +255686957255.  

BlogSpot:matangazombeya.blogspot.com,Email:matangazombeya@yahoo.com/Face:Book:matangazombeya@facebook.com. Ofisi zetu zipo Mama John



SALAMU MAALUM ZA SHUKURANI KUTOKA MBEYA YETU BLOG BAADA YA KUPATA USHINDI WA TATU KATIKA HUDUMA ZA MATANGAZO WAKATI WA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI MBEYA.

$
0
0
Cheti  cha ushindi wa Tatu ambacho Mbeya Yetu walikabidhiwa na TASO
Hili ndilo Banda la  Mbeya yetu Blog lililokuwa ndani ya Maonesho ya Nane nane Mbeya.
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog na Mmoja wa wakurugenzi wa Tone Multimedia Company Limited Joseph Mwaisango kulia Akikabidhiwa Cheti cha ushindi wa tatu  cha vyombo vya habari kikanda katika kurusha matukio yote ya Nane nane Jijini Mbeya na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa  Ruvuma Mh. Rajabu Mwambungu  wa Pili Kushoto.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Kilele cha Nane nane Kanda ya nyanda za juu Kusini Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu  wa pili kutoka kushoto aliye ongozana na Mbunge Mstaafu  Dr. Chrisant Mzindakaya wa  kwanza kutoka kushoto pamoja na wageni wengine wakipata maelezo yakina ndani ya Banda la Mbeya yetu katika maonesho ya  Nane nane 
Mgeni Rasmi katika Maonesho ya  Nane nane Kanda ya nyanda za juu Kusini Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu wa Pili kutoka kushoto akipata maelekezo ya Kina kutoka kwa Mtaalam wa maswala ya Mitandao ya Kijamii  Fredy Anthony Njeje wa  kutoka Tone Multimedia Group  Jinsi habari ambazo zipo katika Mtandano wa mbeya yetu zinavyoweza kupatikana pia kupitia simu ya Mkononi kiurahisi zaidi
Mkuu wa Mkowa  wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka katika Banda la Mbeya ambapo alipata Taarifa fupi kuhusu Blog ya Mbeya yetu kutoka kwa Mtaalam wa Mitandao kutoka Tone Multimedia Group Fredy Anthony Njeje kwa Niaba ya Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango
Mtoa Maelezo kutoka Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje wa kwanza kulia akitoa maelezo ya kina kwa   Mkuu wa Mkoa wa  katavi  Mh.Dr Rajab Lutengwe jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi pia unavyosaidia upatikanaji wa habari kwa urahisi kabisa. Pia kuekeza sababu za Kushiriki katika mashindano ya nane nane ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu juu ya mitandao ya kijamii na faida zake hasa upande wa Blogs na matumizi sahihi.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mh. Mussa Zungiza wa kwanza kushoto akitoa neno la Pongezi kwa Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika kwa Blog ya Mbeya yetu.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mh Mussa Zungiza wa Kwanza kushoto akitoa pongezi kwa Tone Multimedia Group kwa kuwa wabunifu hasa walipo anzisha mkakati wa Blogs za Mikoa ambapo kila Mkoa unakuwa na habari yake, pia amesisitiza waandishi wengine na wamiliki wa mitandao ya Kijamii waige mfano kutoka hapa ili kuleta taarifa za uhakika na muhimu kwa jamii kwa ujumla. wa kwanza kutoka kulia ni Venance Matinya na Fredy Anthony Njeje

Wa kwanza kushoto  ni Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari Nchini Tanzania  (UTPC) Kenny Simbaya alipotembelea Banda la Mbeya yetu na kujionea mambo mengi na Jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi

Kutoka Kulia ni Mwandishi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog na Msimamizi wa Mtandao huo ambao unamilikiwa na Tone Multimedia Group ambaye pia ni Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Joseph mwaisango, Gasper Kutoka Ebony FM, Ray Kutoka Ebony FM, Bony Kutoka Ebony FM na Fredy Anthony Njeje Kutoka Tone Multimedia Group .

Mwandishi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog na Msimamizi wa Mtandao huo ambao unamilikiwa na Tone Multimedia Group ambaye pia ni Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Joseph mwaisango wa kwanza kushoto akitoa maelekezo kwa waliotembelea Banda la Mbeya yetu Blog, wa pili kutoka kushoto ni Mmiliki wa Mtandao wa Kajuna Son Blog Cathbert Angelo
 Wa kwanza kushoto ni Fredy Anthony Njeje kutoka Tone Multimedia , Cathbert Angelo Mmiliki wa Mtandao wa Kajuna Son Blog ambaye pia alikuja tembelea Banda la Mbeya yetu pamoja na Mpanji Mtangazaji wa Clouds Tv na Radio Mkoani Mbeya. 
Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) kanda ya Nyanda za juu Kusini, kimeutunuku cheti mtandao wa kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com ambao upo chini ya Tone Multimedia Company Limited kutokana na kuibuka mshindi wa TATU wa kurusha matangazo Kikanda katika maonesho ya Wakulima nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakagale Uyole Jijini Mbeya.

Tuzo hiyo imekuja kutokana na kikosi cha Mtandao huu kuweka kambi katika maonesho hayo na kufanya shughuli za kurusha matangazo moja kwa moja kutoka uwanjani hapo na kuwapagawisha wakulima ambao walipata fursa ya kutembelea banda letu na kujionea habari zilizotokea muda huo huo na kuonekjana hewani.

Mbali na wakulima na watu mbali mbali waliokuwepo uwanjani hapo pia viongozi wa Taso na wakuu wa Mikoa pia walipata fursa ya kutembelea banda la Mtandao huu katika ziara zao za kukagua mabanda na hivyo kutoa sifa kwa wamiliki wa Mtandao huu namna habari zilivyokuwa zikienda kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Rajab Rutengwe  ambaye ndiye alikiwa wa kwanza   Kwanza kufanya ziara hiyo na kukuta habari zake tokea akipokelea mlangoni hadi kufikia mabanda habari zilikuwa hewani, aliupongeza mtandao wa huu na kusema kwamba inatakiwa watu tubadirike na kwenda na wakati hasa kutumia Fursa za mitandao ya kijamii. Mwingine alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro ambaye pia alijionea na kupata Maelezo Jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyo fanya kazi pia alitoa Pongezi zake kwa kazi kubwa inayofanywa na kutoa habari zenye uhakika zaidi. 

Mgeni Rasmi wakati wa Kilele cha Nane nane mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Rajab Mwambungu amesema wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini wanatakiwa kutumia nafasi waliyonayo kutangaza utanzania na uzalendo wao ndani na nje ya Nchi, Pia aliomba waandishi waige mfano wa Mbeya yetu Blog.

Wageni wengine waliotembelea katika Banda la Mbeya yetu ni Mkurugenzi wa Jiji Mbeya Mh. Mussa Zungiza , na Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari Nchini (UTPC) Kenny Simbaya.

Aidha kufuatia mchango huo wa Taso na wakulima kwa ujumla Uongozi wa Tone Multimedia Group Kupitia  Mbeya Yetu Blog unatoa shukrani kwa wote waliuofanikisha shughuli za Nanenane hadi zinafikia kilele Agosti 8,  na kupelekea kupata cheti cha ushindi.
Tunapenda kuwashukuru TASO kwa namna ya pekee , SBC (T) Ltd kupitia kinywaji chao cha Pepsi na wengine wengi ambao hatutaweza kuwataja majina lakini tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja.

Pia tunapenda kuwashukuru Bloggers wote na waandishi wa habari kwa ujumla hatutaweza kutaja kila chombo lakini tumekuwa pamoja mpaka kufanikisha yote haya.

Mwisho kabisa Tunapenda kukushukuru wewe Mdau wetu Mkubwa wa Mbeya yetu Blog kwa kuonesha Moyo na Kutembelea kila wakati mtandao huu, Tunasema asanteni sana, Bila nyie sisi hatuwezi fanya kazi.

KWA PAMOJA TUUPENDE MKOA WETU WA MBEYA, KUPITIA MTANDAO WA MBEYA YETU BLOG.


MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI LA MCHANGA LILILO PINDUKA NA KUPARAMIA UKUTA NYUMBA YA MTU .

$
0
0
 Lori la Mchanga linalomilikiwa na kampuni ya CCC ambalo namba zake hazikuonekana mara moja Muda mchache baada ya kupata ajali
 Dereva wa Gari hili aliye Tambulika kwa jina la Victor alifariki papo hapo.
 Mashuhuda wakishuhudia Ajali hiyo
 Gari hilo la Mchanga likiwa limeruka eneo hilo mpaka kuparamia ukuta na Kupinduka
 Utaratibu wa kulinyanyua Gari hilo unafanyika
 Hapo ndipo Gari hilo lililokuwa na Kifusi liliruka mpaka upande wa uzio wa nyumba na Kupinduka
 Kushoto ni Baadhi ya Wachina wafanyakazi wa Kampuni ya CCC


 Mmoja wa wafanyakazi akitoka kuangalia Ajali hiyo
Picha na   Mdau wa Mbeya yetu David Nyembe

BREAKING NEWS : SHITAMBALA AMBAYE NI MNEC AMESHIKIRIWA NA POLISI , KUFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO.

$
0
0

Kwa taarifa zilizotufikia muda huu zinasema kwamba Shitambala ambaye ni MNEC kupitia Wilaya ya Mbeya mjini anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kisa kuwatetea wananchi kuhusu Mzungu kuvamia eneo kufikishwa mahakamani kesho...habari kamili endelea kututembelea hapa.


MWANASHERIA NA WAKILI MAARUFU MBEYA APANDISHWA KIZIMBANI.

$
0
0
Picha na Rashid Mkwinda Blog
WAKILI wa kujitegemea mkoani Mbeya na mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa(MNEC) Sambwee Sitambala (42)amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Mfawidhi wilaya ya Mbeya akituhumiwa kwa makosa mawili.
Shitambala amepandishwa leo akituhumiwa kwa makosa ya kuingia kwa jinai na kujenga nyumba katika viwanja viwili namba 27 na 28 Block BB lililopo eneo la Gombe Uyole Jijini Mbeya.
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, wakili wa serikali, Ahmed Stambuli, alisema kuwa Shitambala anashitakiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai kinyume cha kifungu  namba 79 ya mwaka 2014 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Alisema kuwa mshitakiwa kwa nyakati tofauti kati ya Juni 18, 2012 na Novemba 28, 2013 aliingia na kujenga katika viwanja namba 27 na 28 ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali ya raia wa Tanzania mwenye asili ya kiasia aliyefahamika kwa jina la Jaswinder Palsingh.
Alisema kulingana na mazingira hayo, mshitakiwa amesababisha maudhi kwa mmiliki wa kiwanja hicho Palsingh na hivyo kushitakiwa kwa kosa la jinai.
Shitambala ambaye alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo Hakimu Ndeuruo alisema kuwa dhamana ya Mshitakiwa iko wazi ikiwa atatimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja na ahadi ya fedha kiasi cha sh. milioni 1.
Kwa upande wake wakili wa serikali Stambuli alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba iko tayari kuanza kusikilizwa na kuiomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo.
Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.
Akizungumza nje ya mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili anayemtetea Shitambala,Luambano alisema kuwa kesi hiyo imefika hapo kutokana na maslahi ya baadhi ya watu na kuwa kisheria kesi za aina hiyo zinapaswa kusomwa katika mahakama ya Ardhi.

Alisema kuwa mteja amejenga katika eneo ambalo wamejenga watu wengine wapatao 400 na kuwa hata hivyo kesi hiyo imemhusu mteja wake pekee hali ambayo inaonesha nia mbaya iliyofanywa na mlalamikaji dhidi ya mteja wake.

Na  Mbeya yetu 

KUMBE KITUO CHA MIZANI MPEMBA NI KAMA MIKESE . TAZAMA HII CHENI.

$
0
0
 Hapa ilikuwa hakuna Gari kwenda mbele wala  kurudi nyuma
 Wengine wakaanza kuchepuka 
 Jamaa Baada ya kuchepuka akakwama hapa..

Picha na Mbeya yetu

MADIWANI CHUNYA WAWAOMBEA WANANCHI WAO KONDOMU.

$
0
0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Kapala Chakupewa Makelele akifungua mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika jana wilayani hapo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,Charles Mwakalila akisoma ajenda za Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya, Sosthenes Mayoka, akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Chunya.
 Madiwani na wakuu wa idara wakifuatilia kwa makini Mkutano wa baraza la Madiwani wa Wilaya ya Chunya uliofanyika jana.

**********************************
 
KATIKA kuhakikisha gonjwa la Ukimwi halisambai kwa kasi miongoni mwa Wananchi, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameitaka Serikali kuongeza Kondomu katika maeneo ya mikusanyiko.
 
Madiwani hao walitoa rai hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, ambapo walisema katika maeneo ya Mfwenkenya, Lupa na Namsinde yana kiwango kikubwa cha maambukizi.
 
Walisema ili kunusuru hali hiyo ni bora Kondomu zikasambazwa za kutosha katika maeneo hayo ama kuwaruhusu wafanyabiashara kuuza kwa wingi katika maduka yao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu jinsi ya kutumia na kujikinga na maambukizi.
 
Waliongeza kuwa maeneo ya ya mikusanyiko ya watu ndiyo inatakiwa kupewa vipaumbele sana kutokana na kuwepo mchanganyiko wa watu wenye tabia tofauti pamoja na mabinti wanaofanya biashara za ngono.
 
Diwani wa kata ya Mbangara, Abrahamu Sambira, alisema hali ya maambukizi inatisha kutokana na mabinti kulazimisha kufanya ngono na wanaume kwa malipo ambapo hufikia hatua ya kuomba hata mahindi kwa mwanaume asiyekuwa na fedha.
 
“ Ndugu zangu hali ni mbaya mabinti wanalazimisha mapenzi ambapo wanakuuliza kuwa kama huna fedha lete hata mahindi hivyo kuifanya shughuli hiyo kama halali wakati ni hatari” alisisitiza Diwani huyo.
 

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dk. Sichalwe alisema suala la upatikanaji wa Kondomu ni kubwa kwa Wilaya nzima hivyo ataendelea kulifanyia kazi ili kunusuru hali hiyo.

Na Mbeya yetu

MBEYA YETU BLOG LEO TUPO MAJENGO

$
0
0
Hapa njia panda kwa Dausen kuelekea  Majengo
Hii mitaa ya Majengo na Mkeka wa Maana ..
Hakuna kukamatwa na vumbi tena
Hapa kilimani Kuelekea Regco Majengo hii.. no vumbi 
Watu mbalimbali wakiendelea na mambo yao mitaa ya Regco
Baadhi ya Barabara mitaa ya Majengo 
Hapa ni Regco penyewe pametulia 
Mitaa ya Majengo huku ambapo  Mbeya yetu imetembelea leo
Baadhi ya maeneo Majengo
Huku ni maeneo makongwe sana Mbeya 
Mitaa
Miundombinu ikiwa imeimarishwa ipasavyo
Hii ni moja ya Njia panda Majengo

Picha zote na Mbeya yetu 

Usikose kesho ....

AJALI WEST STREET GARI MBILI ZAPARUANA IKIWEMO YA SERIKALI NA HIACE MUDA HUU,

MRADI WA KUZUIA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE WAZINDULIWA JIJINI MBEYA

$
0
0

Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Chifoda Yesaya Fungo akizindua Mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia kwa wanawake katika ukumbi wa Halmashauri jiji Mbeya


Mrtibu wa MBEPAU Jane Lawa akitoa maelezo mafupi jinsi mradi huo utakavyofanya kazi kwa kushirikiana wadau mbalimbali katika jamii


Mratibu wa NGOS Victor Kabuye akifafanua zaidi jinsi mradi huo utakavyofanya kazi karibu na jamii 




 

Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga akitoa neno la shukrani kwa waratibu wamradi wa MBEPAU kuwa wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na sasa kazi tu kushirikiana kutokomeza vitendo vya ukatili wa kinjinsia




Baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi huo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi


MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA AKITOA NENO LA SHUKRANI



PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUZINDULIWA KWA MRADI HUO

Picha na Mbeya yetu

JE SOUTH STREET HAIPO KATIKA RAMANI YA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA, HUU NI MTAA MAARUFU.

$
0
0
 Kwanza kibao kimechoka kiasi hiki.. hamkioni jamani
 Mtaa wote Lami isha kwisha kama unavyo onekana
 Madereva si kwamba hawapendi pitisha magari hapa lakini sasa tatizo barabara jamani 
 Hapa sasa panajieleza 
 Wengine wameamua kuweka vipande vya Cement njia ikae sawa 
 Huku Ma defender tuu ndio yanaweza pita .... ina maana jiji hawapiti huku?
 Mashimo huku hatari... Hata gari huwezi kwepesha kabisa kila unapogusa shimo
 Hapa sasa IST, Vitz, na haya magari mengine madogo yanapitaje? 
 Cha kushangaza sasa Hizi ndizo sehemu ambazo watu wanatakiwa kutupa uchafu.... yaani Dust bin
Wadau wa Mbeya na Halmashauri ya Jiji tuongee kidogo hivi kweli hapa mtu akitupa taka, anakuwa anasafisha Jiji ama anaweka kero katika Jiji? 

JE HALMASHAURI YA JIJI HII BARABARA HAIWAHUSU HATA KIDOGO ? AU IMESAHAURIKA TUU!

TOA MAONI YAKO JUU YA HILI...

PICHA NA MBEYA YETU.

TUNAENDELEA NA MAAJABU YA BARABARA ZA MBEYA: WANANCHI WA ISANGA WALIA NA BARABARA HII ILIYOGEUKA KAMA ENEO LA MACHIMBO ! JIJI MBEYA MPO?

$
0
0
 Mashimo ya kutosha katika njia hii...
 Unaweza kusema hili ni Karavati kumbe ni bonge la Shimo
 Hapa si eneo la Machimbo ya Mchanga lakini Barabara imeharibika
 Hapa ni sehemu maalum ya kuangalizia gari, Bajaji, Baiskeli, au Bodaboda kama zimepata Pancha au tatizo lolote kabla ya kuanza safari ya kuingia katika mashimo tena, pia hapa magari mengi hupumzika.
 Hapa Full Mix huwezi jua gari gani linaenda wapi
 Kushoto jamaa mpanda Baiskeli akijihami na spedi mkononi wakati akikatiza katika barabara hiyo
 Hapa hapatamaniki
 Hatari mawe yanayoweza choma Matairi na kusababisha maafa
 Kushoto kulia ... kushoto kulia... tutafika
 Hapa mdau weka Caption yako.....
 Bajaji inakwepa shimo hadi inataka poteza mwelekeo
 Sasa hiii Barabara si Bora ingechimbwa ifahamike tuu kulipo kama inavyo onekana hapa sasa

 Sasa wengine wamehamishia Dampo

SWALI LINABAKI PALE PALE, JE ENEO HILI LA ISANGA HALIPO KATIKA RAMANI YA JIJI LA MBEYA?

KWA MAONI YETU KAMA MBEYA YETU, TUNAISHAURI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA KUMUOMBA MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA MBEYA-LWANJILO KAMA WALIVYOFANYA META-STENDI KUU.

TOA MAONI YAKO JUU YA HILI.

PICHA NA MBEYA YETU

TRAFFIC MPO! MNAIONA HII IMESHAFIKA SAE KUTOKA SOWETO!

$
0
0

Vijana wakiwa wanasukuma wakitokea Soweto
 Kulia jamaa wakiwa wanashangaa tuu
Haoo.... Mwendo Mdundo
Sasa hapa wapo Sae.. Safari inaendelea 

Picha na Mbeya yetu

KUTOKA JIJI LA MBEYA JIONI HII.. WANAFUNZI BAADA YA MASOMO SASA WANAREJEA NYUMBANI


MBEYA YETU LEO IMEMULIKA BARABARA KOROFI AMBAYO VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU NA WATUMISHI WA SERIKALI HUITUMIA KWA KIASI KIKUBWA.

$
0
0
Hiki ni kipande kifupi sana cha barabara ambacho hakina hata Robo Kilometa , kipande hiki cha barabara ni Muhimu sana kwa sababu Magari ya Mahakama Kuu yanapita hapa, Mahabusu wanapopelekwa Mahakamani wanapitishwa hapa, RPC anapita hapa, Majaji wanapita hapa, Wanasheria wa Serikali wanapita hapa, Benki kuu wanapita hapa, wanafunzi na wananchi wanapita hapa. Lakini cha kushangaza na kustaabisha zaidi kakipande haka ka Barabara kamesahaulika kabisa hakuna anayekitazama ni miaka kadhaa imepita hakuna ukarabati wowote.
Kwa wahusika wa Miundo Mbinu ya Barabara Jiji la Mbeya hivi Kero hii mnaiona
Hiki ni kilima ambapo Mbele jengo kubwa la Ghorofa ni Mahakama Kuu kanda ya nyanda za juu kusini , hapo hapo ndipo unaelekea Benki kuu na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Lakini Barabara ndio kama inavyo onekana.
 Hili ni Moja ya Korongo kubwa ambalo lipo katika kipande hicho cha barabara 
 Hapa pana Afadhali kidogo
 Haka kasehemu kamechimbika 
 Hapa hakuna hata pakukwepea
 Hakuna unafuu eneo hili
 Makorongo mwanzo mwisho
 Magari yanapishana kwa Shida.

USHAURI KUTOKA MBEYA YETU, WAKATI JIJI WANAENDELEA KUJIPANGA KATIKA HILI BASI CHUO CHA MAFUNZO  MAGEREZA KAMA KUNA WAKANDARASI WASAIDIE BASI HATA KUWEKA KIFUSI HAPO.

Picha zote na Mbeya yetu


NEWS ALERT: MBEYA YETU SAFARINI TUKUYU, KAA MKAO WA 'SURPRISE'

$
0
0
Kikosi kazi cha Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa mtandao wa Mbeya yetu Blog chini ya Blogs za Mikoa yaani sasa Tumedhamilia kwa nia moja kutembelea Wilaya ya Rungwe - Tukuyu  kutazama fursa mbalimbali ambazo watu wengi hawazifahamu, kutazama shughuli mbalimbali na mambo mengi. 
Safari hii ambayo imeandaliwa na sisi wenyewe itagusa hisia za wengi  na kila mmoja kwa nafasi yake.. Hii ni nafasi yako Mwana Mbeya na unayesoma na upo nje au ndani ya Tanzania Tegemea mengi...
Kaa mkao wa Kujua Mengi usiyo yafahamu Kuhusu Wilaya ya Rungwe -Tukuyu na Maeneo yake.... Hii ni Fursa yako wewe Mtanzania ambaye upo ndani na nje ya Tanzania kujionea mengi.. hii itakuwa ni 'Surprise' kwenu

Picha na Mbeya yetu.

MBEPAU YAZINDUA MRADI KUHUSU KUZUIA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE MBEYA VIJIJINI.

$
0
0
  Mkurugenzi wa MBEPAU, Jane Lawa, akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 Mjumbe wa bodi ya MBEPAU, Philimon Mwansasu, akimkaribisha mgeni rasmi, wakati wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 Mgeni rasmi,Afisa Tarafa ya Usongwe, Felix Lyaniva, akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya kutambulisha mradi wakifuatilia kwa makini.
Picha ya pamoja baada ya semina.
 
KITUO cha Msaada wa kisheria kwa wanawake(MBEPAU) kimezindua mradi mpya kuhusu kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wanawake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 
Utambulisho wa mradi huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Royal Tughimbe uliopo Mbalizi na kuwashirikisha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ambao ni viongozi wa dini, watendaji wa Kata, viongozi na mila na watu mashuhuri.
 
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika utambulisho huo, Mkurugenzi wa MBEPAU, Jane Lawa, alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ilikuwa ni kuwasadia wanawake na watoto katika sheria zinazowabagua na kuwakandamiza.
 
Alisema pia kupitia MBEPAU wanawake na watoto wanaweza kuzitambua sheria na kuzilinda na kuzitetea haki zao baada ya kuzifahamu na kuzitambua.
 
Aliongeza kuwa hayo yote yametokana na gharama kubwa ya Wanasheria katika kushughulikia malalamiko yanayopelekwa wanawake wengi wasiojiweza na utaratibu wa kutoza fedha kabla ya huduma ufanywao na wanasheria.
 
Mama Lawa alisema katika Mradi huo mpya chini ya ufadhili wa Legal Services Facility(LSF) ya nchini Denmark utafanyika kwa miezi 30 kwa gharama ya shilingi Milioni 200.
 
Alisema malengo ya Mradi ni kuongeza ufikiaji wa huduma za kisheria kwa wanawake na wanaume wilayani Mbeya, kuwajasirisha  wanawake kuweza kutumia mifumo ya kulinda haki zao na kuongeza mwitikio wa jamii katika kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani Mbeya.
 
Alisema kutokana na mradi huo wasaidizi wa kisheria 50 wamepata mafunzo juu ya ulinzi wa haki za wanawake na utoaji wa huduma za kisheria kwa Halmashauri za wilaya Mbeya na Jiji.
 
Aliongeza kuwa viongozi 50 wa jadi, kisiasa na dini pia wamepata mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na utambulisho wa mradi kwa wadau 80 kutoka Halmashauri ya wilaya Mbeya na Jiji.
 
Awali akizindua mradi huo, Mgeni rasmi wa tukio hilo, Katibu Tarafa wa tarafa ya Usongwe, Felix Lyaniva, alilipongeza Shirika la MBEPAU kwa juhudi zao za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa kipaumbele kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 
Alisema ili juhudi hizo ziendelee kuungwa mkono ni vema washiriki wa Semina hiyo wakafikisha elimu kwa wananchi katika ngazi za chini ili wawe na uelewa juu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na msaada wa kisheria.
 
Aidha alitoa wito kwa Wamiliki wa Asasi za kiraia kufikisha huduma zao vijijini kwa kuwa wanaowalenga zaidi ni wanawake na watoto waishio vijijini hivyo ni bora kujenga ofisi huko huko kuliko kujikita mijini tu.

Na Mbeya yetu
 

BREAKING NEWS: LORI LAFELI BREKI KATIKA MLIMA MBALIZI NA KUSABABISHA AJALI MBAYA YA KUGONGA MAGARI MATATU., WATU ZAIDI YA KUMI WAJERUHIWA.

$
0
0



















TAARIFA KAMILI BAADAE
PICHA NA MBEYA YETU

WAANDISHI WA HABARI MBEYA WAISHUKIA TMF

$
0
0
Afisa Ruzuku kutoka TMF akifungua semina kwa waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Washiriki wa semina wakiwemo maafisa wa TMF na Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa makini

BAADHI ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wametoa duku duku lao kwa Mfuko wa vyombo vya habari nchini(TMF) kuhusu utaratibu wa kupata ruzuku kwa ajili ya kufanya kazi za uchunguzi.
Malalamiko hayo yalitolewa jana mbele ya viongozi wa TMF katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa GR Hotel iliyopo Soweto jijini Mbeya ambapo waandishi wa Habari walipata fursa ya kutoa ya moyoni.
Awali Afisa Ruzuku wa TMF, Japhet Sanga, katika utangulizi wake aliuliza idadi ya waandishi waliowahi kunufaika na Mfuko huo kwa Mkoa mzima tangu uanzishwe ambapo waandishi sita waliweza kujitokeza.
Kutokana na idadi hizo Afisa huyo alizidi kuhoji ni kwanini idadi iwe ndogo kiasi hicho ukilinganisha na utitili wa Waandishi wa Habari uliopo Mkoa wa Mbeya.
Wakichangia hoja baadhi ya waandishi walisema wanahisi kuwepo kwa hali ya upendeleo kwa baadhi ya waandishi kujirudia kupata ruzuku aidha kwa kuangalia majina ama kupata chochote kutoka kwa mwandishi(ten percent).
Hata hivyo changamoto nyingi zilizozungumzwa na Wanahabari, Afisa Ruzuku alisema zimechukuliwa na kufanyiwa kazi kisha kuendelea na ufafanuzi juu ya namna ya kuomba ruzuku kwa kufuata vigezo na masharti.
Na Mbeya yetu Blog
Viewing all 1224 articles
Browse latest View live




Latest Images